Tennis

Novak Djokovic ahofia mchezo wa tenisi kupoteza umaarufu

LONDON: MCHEZA tenisi maarufu duniani Novak Djokovic ameonya kwamba tenisi huenda ikapoteza ufalme wake katika michezo ya raketi kutokana na ongezeko la aina mbalimbali za michezo ya aina hiyo hasa inayochezwa maeneo ya nje ya miji.

Djokovic mwenye miaka 37, alisema hakuna juhudi za kutosha kufanya tenisi iweze kufikiwa au inayoweza kumudu jambo ambalo limeiacha hatarini katika ngazi ya klabu.

Bingwa huyo mara saba wa Wimbledon anahofia tenisi kuwa hatarini kwani umekuwa kiungo kikubwa kati ya tenisi na squash unaochezwa kwenye viwanja vidogo vya ndani na mipira laini ambapo unatumikia kwa mikono na unaweza kutumia kuta.

Zaidi ya watu milioni 30 wanashindana duniani kote na mashabiki ni pamoja na Andy Murray, David Beckham na Annabel Croft.
Amesema michezo hiyo inayochezwa nje na bila kuta pia inatia changamoto utawala wa tenisi huku Kim Kardashian akiwa miongoni mwa wafuasi maarufu.

Related Articles

Back to top button