Tennis

Medvedev kucheza na bingwa mtetezi kesho

LONDON, Uingereza: MCHEZAJI tenisi wa kirusi Daniil Medvedev baada ya kumuondoa mchezaji nambari moja wa Dunia, Jannik Sinner katika mashindano ya Wimbledon, kesho Julai 12 anatarajiwa kucheza na bingwa mtetezi wa mashindano hayo Carlos Alcaraz.

Medvedev alimuondoa bingwa namba moja wa Sinner katika pambano lao mzunguko wa seti tano.

Ushindi wa Medvedev ni kama kulipiza kisasi kwa Sinner baada ya kushindwa kwake katika fainali ya Australian Open ambapo alipoteza mfululizo mechi tano dhidi ya Sinner.

Katika seti ya tatu ya mchezo huo Sinner, alishinda kuendelea baada ya kujisikia vibaya akidai alihisi kizunguzungu ambapo alikwenda nje ya uwanja kwa ajili ya matibabu.

Sinner alisema aliingia katika mchezo huo akiwa hajisikii vizuri kiafya pamoja na uchovu aliokuwa nao huku akidai hakutapika kipindi alipokuwa akijisikia vibaya lakini alipumzika kwa kuwa hakuwa akijisikia vizuri.

“Sikuwa vizuri, sikutapika bali nilichukua muda kwa sababu nilikuwa na kizunguzungu. ‘Haikuwa rahisi kwangu kuendelea kucheza lakini nilijaribu kucheza lakini sikushinda,’ amesema.

Related Articles

Back to top button