La Liga

Cubarsi: kinda wa Barca kwenye viatu vya Kompany

BARCELONA: Kocha wa Bayern Munich Vincent Kompany amemtaja mlinzi wa kati wa FC Barcelona Pau Cubarsi kama mchezaji bora na tishio zaidi siku zijazo.

Kompany anajiandaa kwa mtihani mgumu zaidi katika kipindi chake cha ukocha hadi sasa anapojiandaa kuivaa Barcelona iliyojaa vipaji vichanga vya vijana kama Cubarsi usiku wa leo.

Akiwa anatambulika sana kama mmoja wa mabeki bora wa kati wa kizazi chake, Kompany alikiri anatarajia Cubarsi kufuata nyayo zake ikiwa naye alianza career yake akiwa na umri mdogo.

“Atakuwa miongoni mwa mabeki wa kati wazuri sana, atakuwa kiongozi katika eneo hilo. Sio tu kuichezea Barca, lakini katika kiwango cha ari aliyonayo kwa umri wake ni kipaji kikubwa na nadra sana”.

“Nilibahatika kuanza soka mdogo sana, lakini sio kwa kiwango hiki. Sio tu kwa sababu anacheza Barca, lakini kwa sababu yuko kwenye timu yenye ubora wa hali ya juu. Ikiwa hataandamwa na majerahi, atakuwa mchezaji mkubwa.” amesema Kompany

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button