La Liga

Mbappe aeleza kwanini hakumvua jezi namba10 Modric

Madrid: HISPANIA: MCHEZAJI mpya wa Real Madrid, Kylian Mbappe, amesema hakuchukua jezi namba 10 inayovaliwa na Luka Modric kwa kuwa anamheshimu mchezaji huyo kwa umri na uwezo wake ndiyo maana alishinda tuzo ya Ballon d’Or.

“Sijawahi kusema nataka jezi namba10 nafahamu hiyo ni namba ya Luka Modrić. “Ninaheshimu kucheza na Modric. Yeye ni bingwa wa Ballon d’Or na ninamheshimu sana,” alieleza Mbappe.

Mbappe alitambulishwa rasmi na wababe hao wa LaLiga jana mbele ya mashabiki waliojaa katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anasajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuondoka Paris Saint-Germain ambapo alikuwa akivalia jezi namba 7 huku akitumia jezi namaba 10 timu ya taifa ya Ufaransa.

Mbape amechagua kuvaa jezi namba 9 akiwa Madrid na namba 10 itaendelea kuvaliwa na Luka Modric anayedhaniwa kuwa huenda ukawa msimu wake wa mwisho katika ligi huko Uhispania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button