Kepa kurudi darajani
BAADA ya kudaka michezo 12 akiwa Real Madrid kwenye La Liga, na michezo minne ya Ligi ya Mabingwa, imeripotiwa Kepa Arrizabalaga, 29, huenda akarejea Chelsea.
Agosti 14, 2023 Chelsea ilimtoa Mhispania huyo kwa mkopo kwenda Real Madrid ambapo baada ya kufika amekutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Andriy Lunin baada ya Thibaut Courtois kuumia.
Kwa mujibu Fabrizio Romano, Real Madrid wanataka kuongeza mkataba wa Lunin na wanaendelea kumsubiri Courtois msimu wa joto.
Chelsea ilimsajili Kepa mwaka 2015 akitokea Athletic Club nchini Hispania kwa dau la £71.6m lililovunja rekodi ya makipa ghali zaidi duniani, likipita dau la £67m la Allison Becker wa Liverpool aliyesajiliwa mwaka 2016 akitokea AS Roma.
Katika orodha hiyo kipa wa Manchester United anakaa namba tatu katika makipa ghali duniani zikitumika €55m kumtoa Inter Milan msimu wa 2023.