Ligi Kuu

Coastal Union wafunguka kukimbilia Arusha

UONGOZI wa Coastal Union umetaja sababu tano za kutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kuwa uwanja wa nyumbani wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kupitia taarifa ya klabu hiyo imeweka wazi kuwa wamethamini pendekezo la wanachama na mashabiki wao, kuibakisha timu katika Kanda ya Kaskazini.

“Tunathamini kazi kubwa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwa kuinua Kanda yetu ya Kaskazini kupitia Jiji la Arusha, ombi la muda mrefu la wana Arusha.

Tukiwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid tuna uhakika wa kupata alama tatu kwenye mechi zetu za nyumbani,” ilisema taarifa hiyo.

Coastal Union awali walikuwa wakitumia Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge kabla ya kuhamia katika dimba na Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button