Habari Mpya

Chama : kombe la Toyota limetuamsha

AFRIKA KUSINI: BAADA ya kutwaa kombe la mashindano ya Toyota nchini Afrika Kusini, Kiungo wa Yanga, Clatous Chama amesema kombe hilo litawaongezea morali ya kufanya vizuri kwa msimu mpya wa 2024/25.

Chama ni kiungo mshambuliaji mpya wa wananchi Yanga ambaye amejiunga na wababe hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani akitokea Simba alipokuwa msimu wa 2023/24 amesema ni furaha kwao kupata ushindi na malengo ni kupata makombe zaidi wanayoshindania.

Yanga ambayo ilikuwa timu alikwa walichukua Kombe hilo baada ya kushinda dhidi ya wenyeji wao Keizer Chiefs ya Afrika ushindi wa mabao 4-0.

“Kwetu kila kitu tunachukulia kwa umuhimu mkubwa, ushindi wetu na kupata kombe hili ni muhimu, tunaamini mwanzo mzuri, tutazidi kupambana kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote mashabiki wazidi kujitokeza uwanjani kushuhudia burudani zaidi.” amesema Chama.

Amesema mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs ulikuwa mzuri, bao la mapema walilopata lilienda kufanya mchezo huo kuwa rahisi na kufanikiwa kupata idadi nyingi ya mabao na kurejea na kombe hilo.

Chama ameongeza kuwa kufanya vizuri na kutwaa kombe hilo, ishara nzuri kwao kwenye mashindano yanayotarajia kuanza na matarajio yao ni kuona wanafanya vizuri mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Simba, Agosti 8, mwaka huu.

Yanga inatarajiwa kurejea Dar kwa ajili ya mwendelezo wa maandalizi ya msimu wa 2024/25 ambapo Agosti 4 2024 inatarajiwa kuwa Wiki ya Mwananchi siku ambayo watafanya utambulisho wa wachezaji wapya na wale ambao walikuwa kwenye kikosi msimu wa 2023/24

Related Articles

Back to top button