‘Ngoma’ ya Lawi sasa inachezwa TFF

DAR ES SALAAM: KATIBU wa Coastal Union, Omary Ayoub amesema shauri la beki wao Lameck Lawi bado lipo chini ya Kamati ya Hadhi na haki za wachezaji inayosimamiwa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.
Ayoub meyasema hayo kando ya kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika makao makuu ya TFF, Karume kujadili masuala mbalimbali ikiwemo haki na uhalali wa Lawi kuwa ni mchezaji wa Simba au anabaki Coastal Union.
Ameiambia Spotileo kuwa waliitwa kwenye kamati na kusikilizwa na wanasubiri maamuzi kutoka kwenye Kamati.
“Tunaimani na hivi vyombo vinavyosimamia, maamuzi ikiamulia mchezaji aende Simba bure bila Coastal Union kupata chochote tutaridhia, pia tukiambiwa Lawi abaki basi hatuna pingamizi, tunaimani na kamati,” amesema Katibu huyo.
Kwa upande wa Simba waliowakilishwa na wanasheria wao ambao baada ya kumaliza kusikilizwa kwa shauri lao waliondoka huku Kamati ikiendelea kusikiliza mashauri mengine yaliyofika mezani kwao.