Habari Mpya

Nzengeli aipeleka Yanga fainali

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Yanga, Maxi Nzengeli ameipeleka Yanga kucheza fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kufunga bao pekee dakika ya 44 katika mchezo wa Dabi dhidi ya Simba.

Kwa matokeo hayo Yanga itacheza fainali dhidi ya Azam FC waliofanikiwa kumfunga Coastal Union kwenye nusu fainali ya pili uliochezwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, kwa ushindi wa mabao 5 -2.

Fainali hiyo itachezwa Agosti 11, mwaka huu katika dimba la Benjamin Mkapa ambapo Azam FC atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button