Burundi inatisha huko FIBA Africa U16 championship
KIBAHA PWANI: TIMU ya Taifa ya Burundi ya wavulana wametinga fainali ya mashindano ya Kanda ya tano ya Afrika ya vijana chini ya miaka 16 yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Filbert Bayi, uliopo Kibaha mkoani Pwani.
Timu hiyo ya Burundi ilishinda michezo yake yote miwili ya awali kwa kuwafunga Tanzania kwa vikapu 63 kwa 52 katika mchezo uliochezwa jana na leo vijana hao wakashinda mchezo wa pili dhidi Kenya kwa kushinda vikapu 70 kwa 66.
Burundi inasubiri mshindi wa mchezo wa leo jioni kati ya Kenya dhidi ya Tanzania, watacheza fainali ya kutafuta Bingwa wa mashindano hayo.
Kwa upande wa Wasichana Tanzania, jana ilifanikiwa kushinda mchezo wa kwanza kwa kushinda vikapu 88 kwa 17 kwa kumfunga Burundi.
Timu hiyo ya wasichana wenye umri chini ya miaka 16 itacheza tena kesho mchezo wake wa pili dhidi ya Kenya kwa ajili ya kutafuta bingwa wa mashindano hayo.