KikapuMichezo Mingine
Wababe NBA kutamba kombe la Dunia

NYOTA mbalimbali wanaocheza ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA wanatarajiwa kuipamba michuano ya kombe la dunia la mchezo huo (FIBA World Cup) yatakayoanza mwezi Agost mwaka huu.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agost 25, 2023 hadi septemba 10 huko nchini Ufilipino, Japan na Indonesia na takribani mataifa 32 yatashiriki michuano hiyo.
Wachezaji waliotamba kwa vipindi tofauti katika NBA wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo akiwemo Joel Embiid wa Cameroon, staa wa mabingwa wa msimu uliopita Denver Nuggets Nikola Jokic raia wa Serbia na Giannid Antetokounmpo wa Ugiriki miongoni mwa wengine.