EPL

Bentancur kuikosa United kesho

LONDON, ENGLAND: Kiungo wa Tottenham Hotspur, Rodrigo Bentancur hatakuwa sehemu ya mchezo wa kombe la ligi (Carabao Cup) dhidi ya Manchester United baada ya kiungo huyo kushindwa rufaa yake kupinga adhabu ya kufungiwa mechi saba baada ya kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya mchezaji mwenzie Son Heung-Min.

Kamati ya udhibiti wa wachezaji ya chama cha soka nchini England ilimfungia Bentancur mechi saba kwa kosa hilo kabla ya nyota huyo kukata rufaa ya kutaka kupunguziwa adhabu hiyo hadi mechi 3 kwakuwa amemuomba Son radhi na amekubali.

Taarifa iliyotolewa na chama cha soka nchini England FA imesema adhabu ya kiungo huyo itaendelea kama ilivyotolewa na kamati ya udhibiti wa wachezaji ya ligi hiyo pendwa Duniani.

Tottenham watakuwa nyumbani katika mchezo muhimu wa robo fainali dhidi ya Manchester United kwenye kombe la ligi (Carabao Cup) kesho Desemba 19 majira ya saa 5 usiku saa za Afrika Mashariki.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button