EPL

Guardiola: De Bruyne, Nathan Ake bado kwanza

WOLVEHAMPTON: Meneja wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City, Pep Guardiola amesema nyota wake wawili kiungo Kevin De Bruyne na beki Nathan Ake hawatakuwa sehemu ya mchezo wa jumapili ugenini dhidi ya Wolves.

Pep ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Molineux Stadium jumapili saa 10 jioni

“Wanafanya mazoezi, na jana Nathan alifanya mazoezi yake ya kwanza na timu. Labda wanaweza kusafiri lakini kuanza hawako tayari”. amesema Pep

De Bruyne amekuwa nje ya uwanja kwa takriban mwezi mmoja baada ya kutolewa katika mechi ya ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Serie A Inter Milan kutokana na jeraha la nyama la paja.

Wakati Nathan Ake amekosekana tangu alipopata jeraha kama hilo mwezi Septemba akiwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Ubelgiji kwenye mechi dhidi ya Uholanzi.

Manchester City ambao ni wa pili kwenye msimamo wa ligi nyuma ya Liverpool wanakutana na Wolves ambao wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa wamefanikiwa kupata pointi moja tu tangu kuanza kwa msimu huu.

Related Articles

Back to top button