Filamu

Bajeti tuzo za Kalasha yapunguzwa

NAIROBI: BAJETI ya Tume ya Filamu ya Kenya imepunguzwa kwa kiasi kikubwa kutoka Shilingi milioni 442 za Kenya hadi milioni 104 katika mwaka wa kifedha, na kuacha nafasi ndogo ya ufadhili wa program mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Filamu ya Kenya (KFC) Timothy Owase amesisitiza kuwa Tuzo za Kimataifa za Filamu na Televisheni za Kalasha 2025 zitafanyika, ingawa vyanzo ndani ya tume hiyo vinasema hakuna ufadhili wa kutosha.

“Bado tunajipanga kwa ajili ya Tuzo za Kalasha. Kukitokea mabadiliko yoyote, shirika litatoa taarifa,” Bw Owase amesema.

Ingawa Owase anaendelea kusisitiza tuzo hizo za kila mwaka zitafdanyika kwa ukubwa na kupendeza mno, ukweli unaonyesha vinginevyo, kwani vyanzo kadhaa vya Tume hiyo vinadai kutokuwa na bajeti ya kuendelesaha miradi yake ikiwemo tamasha la siku tatu la tuzo hizo.

Katika mwaka wa kifedha wa 2023/24, KFC ilipokea Sh442,729,293, kutoka Sh310,052,499 za mwaka uliotangulia, kulingana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu iliyoyolewa Aprili 17, 2024.

Kwa mwaka wa kifedha wa 2024/2025, bajeti ya KFC ilipunguzwa hadi Sh104 milioni, na kuifanya tume hiyo kuhangaika kufadhili programu zake katika tasnia ya filamu.

“Kile tulichotengewa katika mwaka huu wa fedha kinatosha tu kuendesha shughuli za ofisi na kulipa mishahara ya wafanyakazi,” Chanzo chenye nafasi kubwa ndani ya Tume hiyo kiliiambia The EastAfrican.

Kuandaa tamasha hilo la siku tatu inachukua angalau miezi mitatu ya kufanya maandalizi yenye mafanikio lakini hilo bado hayafanyiki hadi sasa.

Jambo linguine linalohashiria kutofanyika kwa tamasha hilo kwa mwaka huu ni kwamba KFC huwa inawaita hadharani watengenezaji filamu kuanzia Novemba kwa ajili ya kuwasilisha kazi zao kabla ya hafla ya Machi mwaka unaofuata lakini haikufanya hivyo hadi sasa.

Kwa mwaka jana KFC milioni 30 za Kenya hutumika kuandaa tamasha la siku tatu la Kalasha International Film & TV Market na tuzo za Kalasha.

Related Articles

Back to top button