Filamu

Filamu ya Ranveer Singh yakutana na ushindani sokoni

INDIA: Filamu mpya ya muigizaji wa India Ranveer Singh inayojulikana kama ‘Dhurandhar 2’’ inatarajiwa kukutana na ushindani mkali katika soko la filamu baada ya kupangwa kuachiwa siku moja na filamu ya Pawan Kalyan, ‘Ustaad Bhagat Singh’.

Hapo awali, filamu ya Yash iitwayo ‘Toxic ‘ ilikuwa itolewe Machi 19, lakini iliahirishwa hadi Juni 4, hatua iliyofungua nafasi kwa filamu ya ‘Ustaad Bhagat Singh’ kuachiwa katika tarehe hiyo.

Wataalamu wa soko la filamu wanaamini kuwa ‘Dhurandhar 2’, iliyoongozwa na Aditya Dhar, inaweza kufanya vizuri zaidi kitaifa kwani sehemu ya kwanza ilikusanya zaidi ya rupia trilioni moja nchini India.

Filamu hiyo pia itatolewa kwa lugha ya Kitelugu kwa watazamaji wa majimbo ya kusini.

Takwimu za awali zinaonyesha kuwa ‘Dhurandhar 2’ tayari imeanza vizuri katika majimbo ya Kitelugu baada ya kuuza tiketi nyingi katika maonesho ya awali, huku pia ikipata zaidi ya dola milioni moja za Marekani katika mauzo ya tiketi za mapema nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button