Filamu

Maiti ya muigizaji wa Hollywood, mkewe yakutwa ndani

MEXICO: MUIGIZAJI wa Marekani aliyeshinda tuzo ya Oscar, Gene Hackman, mkewe Betsy Arakawa na mbwa wao wamekutwa wamekufa nyumbani kwao huko Santa Fe, New Mexico.

Taarifa kutoka kwa Kiongozi wa eneo hilo la Santa Fe huko New Mexico imeeleza: “Tunaweza kuthibitisha kwamba Gene Hackman na mkewe walipatikana wakiwa wamekufa jana Jumatano Februari 16 mwaka huu alasiri kwenye makazi yao huko Sunset Trail.

“Huu ni uchunguzi unaoendelea hata hivyo, kwa wakati huu hatuamini kama kuna mchezo mchafu katika vifo hivyo.” Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Santa Fe iliiambia BBC: “Mnamo Februari 26, 2025 saa 1:45 usiku, manaibu wa maeneo hayo ya Santa Fe walitumwa kwa anwani kwenda Old Sunset Trail huko Hyde Park ambapo Gene Hackman mwenye miaka 95 na mkewe Betsy Arakawa mwenye miaka 64 na mbwa wao walipatikana wakiwa wamekufa.”

Katika taaluma yake iliyochukua zaidi ya miongo sita, Hackman alipokea Tuzo mbili za Academy, Bafta mbili, Golden Globes nne na Tuzo ya Waigizaji wa Screen.

Hackman alishinda mwigizaji bora wa Oscar kwa nafasi yake kama Jimmy Popeye Doyle katika filamu ya kusisimua ya William Friedkin ya 1971 ‘The French Connection’ na nyingine ya mwigizaji msaidizi bora kwa kucheza ‘Little Bill Daggett’ katika filamu ya mwaka 1992.

Hackman amezaliwa California mwaka wa 1930, aliandikishwa jeshini baada ya kusema uongo kuhusu umri wake akiwa na miaka 16, alihudumu jeshini kwa miaka minne na nusu lakini baadae akiwa New York aliamua kuendelea na uigizaji na alijiunga na Pasadena Playhouse huko California.

Hackman na mke wake wa kwanza, Faye Malta, walikuwa pamoja kwa miaka 30 na walilea watoto watatu kabla ya kupeana talaka mnamo 1986.

Related Articles

Back to top button