Filamu

Kim Sharma afunguka kuhusu Shah Rukh Khan

MUMBAI: MUIGIZAJI na muongozaji wa filamu nchini India Kim Sharma amefichua kwamba hakujifunza chochote kutoka kwa waigizaji wenzake Shah Rukh Khan na Amitabh Bachchan, kwa sababu haikuwa kipaumbele chake.

Kim Sharma amesema licha ya kufanya kazi pamoja na magwiji hao wa tasnia ya filamu katika filamu ya ‘Mohabbatein’, lakini hakuna alichoona cha kujifunza na hilo linatokana na sababu kwamba hakuwa akiwafahamu vyema magwiji hao.

“Sikujifunza chochote kwa sababu sikuwa makini. Lazima uelewe hali hiyo: Mfano ukiwa mtoto na Nelson Mandela anapita kama simfahamu, nisingejali. Kwa sababu haikumaanisha chochote kwangu. Nilikuwa mdogo sana kipindi hicho, kwa hivyo sitaita kupoteza muda. Ninaishi maisha yangu bila majuto ni waigizaji wazuri lakini sikuwahi kujifunza kwako kwa sababu sikuwa nikiwazingatia,” ameeleza Kim.

Filamu ya ‘Mohabbatein’ imetayarishwa na Yash Chopra chini ya bendera ya Filamu ya Yash Raj, Mohabbatein katika filamu hiyo amewashirikisha Amitabh Bachchan, Shah Rukh Khan na Aishwarya Rai.

Filamu hiyo kwa sasa inafanya vizuri sana na imekuwa filamu ya India inayoingiza pesa nyingi zaidi kwa mwaka huu ingawa kwa mujibu wa Kim filamu hiyo haikumsaidia kuongeza matarajio yake.

Related Articles

Back to top button