Arteta mitatu tena Arsenal

LONDON: Meneja wa Washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta ameongeza mkataba wa kuendelea kuwafundisha wababe hao wa jiji la London kwa miaka mitatu zaidi
Arteta mwenye miaka 48 ambaye kwa kiasi kikubwa ameibadilisha Arsenal amesaini mkataba huo ambao unatarajia kumuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2027.
Akiwa na Arsenal katika msimu wake wa kwanza kama kocha aliiisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la FA mwaka 2020 na kushinda ngao mbili za jamii mwaka 2020 na 2022
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Arteta amesema maisha yake klabuni hapo ni ya furaha sana na anajivunia mafanikio aliyoyaleta klabuni hapo.
“Ninajisikia fahari sana, kufurahishwa sana na ninatazamia kitakachofuata. Ninajivunia kuwa hapa nilipo na kuwa na uhusiano nilionao na kila mtu katika klabu.
“Ninajihisi mwenye bahati sana kufanya kazi kila siku na watu wazuri na matamanio tuliyo nayo hapa. Najisikia kuhamasishwa sana, ninauhisi uungwaji mkono na ninataka kufanya mengi zaidi kuliko yale ambayo tayari tumefanya pamoja.
Arteta ameiongoza Arsenal katika michezo 175, akishinda michezo 105 sawa na asilimia 60% ya michezo yote. Chini yake Arsenal imefunga mabao 332 ikikusanya wastani wa pointi 1.96 kwa kila mechi.