EPL

Evra:Mrudishieni Maguire kitambaa cha unahodha

LAS VEGAS: Beki wa kushoto wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra ameishauri Manchester United kumpa Harry Maguire kitambaa cha unahodha badala ya Bruno Fernandes.

Maisha ya beki huyo yalirejea kwenye mstari baada ya kipindi kigumu alipopoteza unahodha na nafasi yake kwenye kikosi cha Man United.

Maguire alipoteza nafasi yake kwenye timu ya Manchester United msimu wa 2022/23 chini ya Erik ten Hag. Wengine aliowapendekeza ni Lisandro Martinez na Raphael Varane.

Katika msimu wa joto wa 2023, wababe hao wa Kiingereza walikubali ombi kutoka kwa West Ham, lakini mwishowe aliamua kubaki kwenye timu hiyo.

“Nilikuwa tayari kubaki na kupigania nafasi yangu na tuna mabeki wa kati wanne au watano wakuu wa kimataifa na katika klabu hii na ushindani wa nafasi ni mkubwa sana,” alinukuliwa kupitia The Independent.

Licha ya yote hayo, Maguire anachukuliwa kuwa mchezaji muhimu chini ya Ruben Amorim. Kocha huyo wa Ureno alisema wataongeza kandarasi yake kwa mwaka mmoja.

“Mrudishie kitambaa! ‘Baada ya yote ambayo amepitia kuonesha ujasiri na uongozi,” Evra alitoa maoni kwenye chapisho lake la Instagram.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ameanza mechi nne za mwisho za United na atakuwa mmoja wa majina ya kwanza kwenye mechi dhidi ya Liverpool. Alivaa kitambaa dhidi ya Newcastle na Everton.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button