Haverts mguu sawa dhidi ya Brighton

LONDON: Meneja wa Washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta amesema mshambuliaji wake Kai Haverts atakuwepo kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya England ugenini dhidi Brighton kesho Jumamosi.
Haverts ambaye aliifungia Arsenal bao pekee la ushindi dhidi ya Ipswich Town aliukosa mchezo dhidi ya Brentford baada ya kupata ugonjwa ambao uliathiri pia wachezaji kadhaa wa kikosi hicho.
Alipoulizwa na wanahabari ikiwa Haverts atakuwepo kwenye mchezo huo Arteta alijibu “Ndio, Nadhani yeye na waliokuwa wanaumwa watakuwa sawa, watafanya mazoezi leo na timu halafu tutaona kama wanaweza kutumika kesho”.
Arsenal ni wa pili kwenye msimamo wa ligi, point 6 nyuma ya Liverpool walio na mchezo mmoja mkononi watajaribu kuwasogelea vinara hao kwa ushindi dhidi ya Brighton walio nafasi ya 10.