EPLKwingineko
Chelsea yakubali kumsajili Fofana kwa Bil 191/-


HATIMAYE Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano ya dili lenye thamani ya pauni milioni 70 sawa na shilingi bilioni 191.8 na Leicester City kwa ajili ya kumsajili beki Wesley Fofana.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21 alitaka aungane na Kocha wa Chelsea yenya makao yake Stamford Bridge, Thomas Tuchel.
Chelsea italipa kiasi hicho cha fedha pamoja na nyongeza kwa ajili ya beki huyo wa kati.
Fofana anaaminika kuwa mmoja wa mabeki bora wa kati vijana katika mpira wa ulaya na kwa muundo wa sasa inaonekana kuwa na safu bora ya ulinzi.
Kalidou Koulibaly ana uzoefu mkubwa na Tuchel pia anaweza kuwatumia Thiago Silva, Cesar Azpilicueta na Trevoh Chalobah wakati Fofana ataongeza uimara katika klabu hiyo mojawapo kubwa zaidi duniani.