EPL

Amorim kumaliza sinema ya Garnacho hivi

MANCHESTER:KOCHA mkuu wa Manchester United Ruben Amorim amesema atakaa chini kuzungumza na winga wa klabu hiyo Alejandro Garnacho baada ya kijana huyo mwenye miaka 20 kupitiliza moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilisha nguo alipofanyiwa mabadiliko mda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza cha mchezo wao dhidi ya Ipswich Town jana Jumanne kutamatika.

Amorim alimtoa raia huyo wa Argentina kisha kumtambulisha mchezoni beki Noussair Mazraoui dakika mbili kabla ya mapumziko kufuatia kupewa kadi nyekundu kwa beki beki mwingine Patrick Dorgu dakika ya 43.

Baada ya kutoka Garnacho alipitiliza moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilisha nguo jambo lililoonekana kama utovu wa nidhamu licha ya winga huyo kuashiria kama alitaka kubadilisha nguo kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na haifahamiki kama alirejea kutazama kipindi cha pili.

“Nitazungumza na Garnacho kuhusu suala hili, niliwaza tubadili mfumo haraka, tucheze 5-3-1 ingekuwa hatari kama angekuwepo kwa sababu kasi yake inamfanya awe mzuri sana kwenye ‘1 V 1’ bila shaka tusingemhitaji ilitubidi kuchagua mtu wa kutoka nje na mimi nilimchagua yeye, lilikuwa chaguo langu” amesema Amorim.

Ikumbukwe mwezi Desemba, Garnacho aliondolewa kwenye kikosi cha dabi dhidi ya Manchester City pamoja na mwenzie Rashford aliye kwa mkopo Aston Villa baada ya kile kocha huyo walichosema kuwa ni kiburi na kutojituma mazoezini. Hata hivyo alirejeshwa haraka kwenye kikosi na Rashford kutolewa kwa mkopo.

Related Articles

Back to top button