Sakata la Kane lamuibua Mmiliki Spurs

MMLIKI wa klabu ya Tottenham Hotspurs Joe Lewis amevunja ukimya na kuamua kulizungumzia sakata la nyota wa kikosi hicho Harry Kane ambaye anawindwa vikali sokoni na bado hajaongeza kandarasi mpya klabuni hapo.
Lewis amesema hayupo tayari kumruhusu nyota huyo kuondoka bure klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika hivyo amemwambia mwenyekiti wa klabu hiyo Dany Levy kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England ikiwa hataki kuongeza mkataba mpya.
Imeripotiwa kuwa Lewis amesema kama kuna timu itafikia dau ambalo Spurs wanalitaka basi wamuuze nyota huyo.
Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich wanamuwinda vikali kane wakiamini atakuwa mrithi sahihi wa mshambuliaji Roberto Lewandowski ambaye tangu kuondoka kwake wanahaha kumpata mrithi wake.
Hata hivyo imeripotiwa kuwa timu kutoka Saudi Arabia zinaandaa dau nono ili kuipata saini ya kinara huyo wa mabao wa muda wote wa timu ya taifa ya England.