Kwingineko

Amka na Samia yainogesha Tanga

Mapokezi ya Rais Samia pambe!

TANGA: Jiji la Tanga limeandaa matembezi maalum  yaliyopewa jina la”amka na Samia “ambayo yatahusisha vikundi vya mazoezi (jogging groups) ikiwa wa ni sehemu ya hamasa ya kumpokea Rais Samia ambaye anatarajiwa kuanza ziara mkoani Tanga hivi karibuni.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha amesema kuwa matembezi hayo ni maalum Kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wananchi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi kwenye kumlaki Rais Samia.

“Rais Samia anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga mnamo Februari 23 mwaka huu hivyo Jiji la Tanga lipo kwenye kampeni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kufanya shamra shamra mbalimbali kama jogging ambayo inakwenda kufanyika Jumamosi ya wiki hii”amesema DC Kubecha .

Amesema kuwa Rais Samia amefanikisha miradi mingi ya maendeleo katika jiji hilo hivyo wanafanya hamasa Ili kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kumlaki Rais.

Vikundi vya jogging sambamba na burudani mbalimbali vitakuepo Ili kunogesha matembezi hayo ambayo yataanza na kumalizika katika viwanja vya CCM Mkwakwani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button