Kwingineko

Kivumbi Dabi ya Manchester fainali FA leo

FAINALI ya Kombe la FA 2023 kati ya Manchester City na Manchester United inafanyika leo kwenye uwanja wa Wembley, London.

Karibu mashabiki elfu-90 wanatarajiwa kujaza uwanja wa Wembley licha ya migomo zaidi ya kitaifa ya wafanyakazi wa treni hivyo kusababisha maelfu ya mashabiki watumie usafiri mbadala kwenda London.

Kocha Mkuu wa City Pep Guardiola ambaye tayari ametwaa taji la Ligi Kuu na ataikabili Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Juni 10 anahitaji ushindi ili kukaribia kunyakua mataji matatu msimu huu.

Lakini United inatafuta kuongeza taji baada ya kutwaa Kombe la Carabao Februari mwaka huu kukamilisha mataji mawili ya ndani.

“Tunataka kushinda kombe, sio kuwazuia. Tuna fursa kubwa. Pengine Wembley ni uwanja bora zaidi duniani na kuwa pale kwenye fainali ya kombe ni jambo la kusisimua sana,” amesema Kocha Mkuu wa United, Erik ten Hag.

Katika mchezo wa mwisho timu hizo kukutana Manchester United iliifunga Manchester City mabao 2-1 ikiwa mechi ya ligi.

Related Articles

Back to top button