Kwingineko
Bento, akubali kumfuata Ronaldo, Al-Nassr

SAUDI Arabia: GOLIKIPA kutoka Brazil, Bento aliyekuwa akihusishwa kuhamia Chelsea ya Uingereza ama Inter Milan ya Italia amekubali kujiunga na Klabu ya Al Nassr anayoitumikia mwanasoka nguli Cristiano Ronaldo.
Kwa mujibu wa mtaalam wa uhamisho wa kandanda Fabrizio Romano, mchezaji huyo mwenye miaka 25 amejiunga na Al-Nassr kwa mkataba wa miaka minne kutoka Atletico Paranaense.
“Rasmi, imethibitishwa. Golikipa wa Brazil Bento ameingia kama mchezaji mpya wa Al Nassr kwa mkataba wa miaka minne,” Romano aliandika kwenye mtandao wa X.
“Bento amesajiliwa kwa kitita cha paundi milioni18.
Bento kwa mara ya kwanza alitua katika kikosi cha Athletico Paranaense akiwa na umri wa miaka 21 mnamo Novemba 2021.