Kwingineko

Al-Ittihad yamtambulisha Kante

MABINGWA wa Ligi Kuu ya kulipwa Saudi Arabia Al-Ittihad imethibitisha kusamjili NG’olo Kante atakapokuwa huru mwisho wa mkataba wake Chelsea mwezi huu.

Kante amekuwa akihusishwa kuhamia Saudi Arabia na sasa klabu hiyo yenye makao yake jiji la Jeddah imethibitisha ikimsifia kiungo huyo mfaransa kuwa ni mkata umeme bora zaidi duniani.

Uthibitisha huo unatamatisha mwisho wa Kante kuitumikia Chelsea, akiwa amejiunga na timu hiyo ya London mwaka 2016 akitokea Leicester City.

Atakipiga na mfaransa mwenzake Karim Benzema kwenye klabu hiyo baada ya kuwa mmoja wa wachezaji wa kigeni wanaokiwasha Ligi ya kulipwa ya Saudi Arabia akiwemo Cristiano Ronaldo anayeitumikia Al-Nassr.

Taarifa Al-Ittihad iliyochapishwa kuthibitisha uhamisho huo imesema: “Klabu ya Ittihad inamtakia mafanikio Kante katika kufikia malengo ya klabu na kutimiza matarajio ya mashabiki na wapenzi wote wakati akiwa na timu yetu.”

Wakati akiitumikia Chelsea na Leicester City, Kante ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na The Blues mwaka 2021.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button