World Cup

Kocha Argentina afikiria kujiuzulu

KOCHA aliyeiwezesha Argentina kutwaa Kombe la Dunia 2022, Lionel Scaloni amesema anafikiria kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuinoa nchi hiyo kwa miaka mitano.

Scaloni ametoa kauli hiyo ya ghafla baada ya Argentina kushinda mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wapinzani wakuu Brazil kwa bao 1-0 Novemba 21 jijini Rio de Janeiro.

Pia kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 aliiongoza Argentina kutwaa Copa Amerika mwaka 2021 kabla ya kunyakua ubingwa wa Dunia nchini Qatar mwaka uliopita.

“Nahitaji kufikiria mengi kuhusu nini nitafanya nini. Nahitaji kufikiria muda huu,’ amesema Scaloni.

Scaloni alichukua nafasi ya Jorge Sampaoli Agosti 2018 baada ya kushika kwa muda mikoba ya timu ya taifa ya vijana chini miaka 20.

Related Articles

Back to top button