LIGI kuu soka Tanzania bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga ni wenyeji wa Polisi Tanzania ya Moshi, Kilimanjaro.
Coastal Union inashika nafasi ya 10 ikiwa pointi 3 baada ya michezo miwili wakati Polisi Tanzania ipo nafasi ya 13 ikiwa pointi 1 baada ya idadi kama hiyo ya michezo.
Katika mchezo wa mwisho kati ya timu hizo wa ligi kuu Mei 8, 2022, Coastal Union iliifunga Polisi Tanzania.




