Ligi Kuu

Pazia la Ligi Kuu kuhitimishwa leo

DAR ES SALAAM: LIGI Kuu Bara inatarajiwa kutamatika leo Juni 30, 2026 ambapo Yanga itakuwa ugenini ikimechuana dhidi ya JKT Tanzania huku Simba ikiikaribisha KMC.

Macho yote yatakuwa kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo kutazamia mchezo huo ambao utaamua hatma ya Yanga.

Yanga inahitaji ushindi au sare tu kutangaza ubingwa wa tano mfululizo kwa maana hiyo iwapo itapoteza huku Simba ikishinda ubingwa utakwenda kwa wekundu wa Msimbazi.

Ikipata sare na Simba ikashinda itafikisha pointi sawa 73 ila kitachowabeba Yanga wataangaliwa kwenye mabao ya kufunga na kufungwa lakini pia, muujiza unaweza kutokea kwa Simba yote kwa yote dakika 90 zitaamua hatma ya kila mmoja.

Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni Coastal Union dhidi ya Pamba Mkwakwani Tanga, Fountain Gate dhidi ya Singida, Mbeya City dhidi ya TRA, Mashujaa dhidi ya Tanzania Prisons, Azam dhidi ya Dodoma na Namungo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Je nani ataungana na KMC kushuka daraja? Ni Mtibwa, Prisons au Mbeya City kazi ipo leo. Je nani atacheza hatua ya mtoano kati yao? Viwanja vya Lake Tanganyika Kigoma, Sokoine jijini Mbeya na Majaliwa vibeba hatma zao.

Related Articles

Back to top button