Ligi Kuu

Yanga Diarra yuko wapi?

DAR ES SALAAM: MASHABIKI wa klabu ya Yanga ni kama wameingia ubaridi baada ya kumuulizia golikipa wa timu hiyo Djigui Diarra kuelekea mchezo wa hapo baadae dhidi ya mabingwa wa zamani wa soka la Tanzania Simba.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Yanga liliwekwa chapisho lenye picha za wachezaji waliokuwa kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba na mashabiki walipoikosa picha ya Diarra wakaanza kuhoji yuko wapi Diarra?

Ikumbukwe golikipa huyo alikuwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Mali na mapema jana kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisema kuna baadhi ya wachezaji ambao bado hawajarejea nchini na wengine ni majeruhi hali iliyowapa shaka mashabiki wa Yanga.

Mashabiki hao wameonesha kuingiwa hofu ikiwa golikipa huyo atakosekana kwenye mchezo wa leo wakiamini ni sababu ya ushindi mara tatu waliopata dhidi ya Simba kwenye michezo iliyopita.

Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Benjamini Mkapa. Mara nyingi mchezo huu wenye hadhi ya nyota tano hutawaliwa na visa vya hapa na pale wenye wanasema ‘Mind game’.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button