Ligi Kuu

Mgunda aingia kwenye 18 za Simba

DAR ES SALAAM: KOCHA Msaidizi wa Simba, Darian Wilken amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.

Kocha Wilken amesema Namungo ni timu nzuri hasa ikichangiwa na kuwa na kocha mpya, (Juma Mgunda) ambaye amewaongezea morali wachezaji wake lakini itakutana na wapinzani bora zaidi.

“Utakuwa mchezo mgumu, Namungo ni imara yenye wachezaji wazoefu na tayari imepata kocha mpya, lakini Simba ni kubwa zaidi na ipo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajiili ya kupata pointi tatu,” amesema Kocha Wilken.

Amesema ratiba ni changamoto wanalazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji. Timu kubwa inajiandaa kupitia nyakati ngumu ili kuonesha ukubwa wao.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kipa wa Simba, Ally Salim amesema kwa upande wao wapo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu.

Amesema Namungo ina wachezaji wazoefu ambao wengi walikuwa nao lakini Simba ni kubwa na pamoja na changamoto zote wapo tayari kwa ajili ya pointi tatu muhimu nyumbani.

“Tupo tayari kwa mchezo , Namungo tuna waheshimu ni timu bora lakini Simba ni bora zaidi na tupo kwa ajili ya kupigania alama tatu,” amesema Ally Salim.

Related Articles

Back to top button