Mastaa

Pinela Justine afunguka Komenti iliyomuumiza zaidi mtandaoni

DAR ES SALAAM: MSANII, Mwanamitindo na mtumishi wa Mungu kutoka Tanzania, Pinela Justine, amesema kuwa moja ya komenti zilizowahi kumuumiza zaidi kwenye mitandao ya kijamii ni madai ya baadhi ya watu kwamba anatumia bangi.

Pinela amesema mara nyingi watu huandika maoni kwenye mitandao bila kutambua kuwa maneno yao yanaweza kuwaumiza wengine kihisia na kuwavunja moyo.

Akizungumza kuhusu suala hilo, amesema:
“Hata kama mnanitukana matusi ninawaelewa, lakini eti siku hizi Pine anavuta bangi? Jamani, mtumishi wa Mungu avute bangi? Shindweni,” amesema Pinela.

Aidha, ametoa wito kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa makini wanapotoa maoni yao, kwani baadhi ya kauli zinaweza kuwa na athari kubwa kwa wahusika kuliko inavyodhaniwa.

Related Articles

Back to top button