Mastaa

Diamond ampa milioni 10 mzee wa Makosa

MSANII wa Bongo Fleva nchini Naseeb Abdul ‘Diamond’ amempa Milioni 10 Mzee Makosa kutoka mkoani Iringa baada ya kuvutiwa na hadithi ya maisha yake.

Mzee Makosa ambaye alisimulia habari ya maisha yake jinsi alivyowahi kuishi akiwa tajiri lakini maisha yake yalibadilika mpaka kuyumba kimaisha.

Diamond amekutana na Mzee Makosa ofisini kwake Wasafi,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam na kumkabidhi kitita hicho cha pesa Ikiwa na lengo la kumuinua tena kimaisha Mzee Makosa.

Mzee Makosa amemshukuru Diamond kwa pesa hiyo na amesema kuwa kiasi hicho cha pesa ataenda kupanda miti mkoani Iringa kwa ajili ya kusaidia jamii.

Mzee huyo alifanya kazi Ulaya na kujipatia kipato kikubwa na kutumia fedha nyingi kusaidia huduma kwa kutafuta madaktari na kufungua hospitali ili watu waweze kupata matibabu. Pia alipanda miti mingi na kuifanya Iringa kuwa ya kijana.

Ameongeza kuwa kutokuwa na elimu ya fedha ndio sababu kubwa iliyopelekea yeye kufilisika.

Related Articles

Back to top button