Filamu

Patrick: Mama yangu ndiye aliyegundua kipaji changu

....Kanumba alinipa fursa ya kwanza

DAR ES SALAAM: MSANII wa filamu Othman Njaidi, maarufu kama Patrick Kanumba, amesema mama yake mzazi, Hidaya Njaidi, ndiye aliyekuwa wa kwanza kutambua kipaji chake cha uigizaji na kuchangia kwa kiasi kikubwa safari yake ya kuingia kwenye tasnia hiyo.

Patrick amesema baada ya mama yake kuona uwezo wake wa kuigiza, alimueleza marehemu Steven Kanumba, ambaye baadaye alimpa nafasi yake ya kwanza kuigiza

Wawili hao walishirikiana katika filamu za Uncle JJ na This Is It, hatua iliyomfungulia milango kwenye tasnia ya filamu.

Amesisitiza kuwa, licha ya kifo cha Steven Kanumba, ataendelea kuwa mtu muhimu katika safari yake ya kisanii kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kumuinua.

Mbali na uigizaji, Patrick amesema pia ana mapenzi makubwa na muziki, akieleza kuwa ni moja ya maeneo ya sanaa anayoyapenda na anayotarajia kuendeleza.

Kwa sasa, Patrick Kanumba na mama yake, Hidaya Njaidi, wote ni waigizaji wanaotambulika nchini, huku Hidaya akiwa na uzoefu wa miaka mingi zaidi katika tasnia ya filamu.

Related Articles

Back to top button