Mastaa

Shilole aula ubalozi

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa bongo fleva Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametambulishwa kama balozi wa mafuta ya Korie huku akihimiza wananchi kuwa makini kwa kununua mafuta yaliyosalama.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati akisaini mkataba wa kuwa balozi Shilole amesema wananchi wakitumia bidhaa zinazotambulika itawasaidia shida inapotokea kuchukua hatua.

“Wananchi tusikurupuke sana kwa kununua mafuta hayana hata lebo wala hayajulikani kwa kuwa ni rahisi bali tuangalie yenye usalama,”amesema.

Shilole amesema mafuta hayo ya Korie ambayo yamekuwa ni ya muda mrefu walikuwa wakiyatumia kupaka mwilini miaka ya zamani.

Meneja Masoko wa Korie Steve Ford amesema wamechagua Shishi kama balozi wao kwa kuwa ni Mama anayepika lakini pia, mtu maarufu.

Related Articles

Back to top button