David Rajabu kuja kivingine

MWANAMUZIKI muziki wa injili, David Rajabu, anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘upendo’ mwishoni mwa wiki hii, ukiwa na lengo la kuhamasisha upendo na mshikamano katika nchi za Afrika Mashariki.
Rajabu, ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, amewaomba mashabiki wa muziki wa injili kumuunga, amesema wimbo huo utapatikana katika majukwaa mbalimbali ya muziki kuanzia Mei 22 mwaka huu.
“Nimekuwa kimya kwa muda mrefu, lakini sasa nimerudi na Upendo. Huu ni wimbo wa kutuweka pamoja watu wote wa Afrika, hasa wa Afrika Mashariki, kwa sababu penye upendo hakuna jambo linaloharibika.
“Kuanzia Ijumaa hii, video ya wimbo huo itapatikana kwenye chaneli yangu ya YouTube na pia itaonekana katika mitandao mbalimbali. Ninaamini utawabariki wengi,” amesema David.




