Burudani

Diana:Sihusiki Bahati kuacha kuimba injili

NAIROBI: MWANAYouTube na mtayarishaji wa maudhui mbalimbali Diana Bahati amefunguka kwamba hakumshawishi mume wake mwanamuziki Bahati kuachana na muziki wa injili na kuingia katika muziki wa kidunia, kwa kuwa yeye ni mtu mzima na anamaamuziki yake katika muziki anaofanya.

“Watu wanasema nimembadilisha, lakini najiuliza, kivipi? Si ni mtu mzima mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yake? Sasa nimembadilisha vipi, niuamuzi wake mwenyewe,” ameeleza Diana.

Diana aliendelea kusisitiza kwamba uhusiano wake na Mungu ni wa kibinafsi. “Nimeokoka kweli. Kwa sababu tu ninafurahia maisha haimaanishi kwamba watu wanapaswa kunihukumu kwa namna ninavyoonekana. Bwana awe mwamuzi wangu.” Ameeleza.

Akizungumza kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi Bahati anasema mahusiano ya kimapenzi ni muhimu mno kwake. “Mapenzi ni muhimu. Pia, kuwa na urafiki na mwenzi wako na kuelewa kuwa ninyi ni watu wawili tofauti husaidia kuvumiliana,
“Kutoelewana katika uhusiano ni kitu kisichoepukika katika ndoa lakini akasisitiza umuhimu wa akili ya kihisia. “Mwanzoni, niliitikia hovyo na nilikuwa nikipaza sauti yangu, lakini baada ya muda, nilitambua kuwa mtulivu kunafaa zaidi hasa kwa vile Bahati pia hapendi kubishana hili limerahisisha kusuluhisha mizozo.” Ameeleza Diana.

Pia Diana ameeleza namna alivyokuwa tegemezi kwa wanaume akiwa na katika uhusiano na wanaume wengi ili kufanikisha maisha yake.

“Nimefanya maamuzi ambayo sijivunii, lakini ni sehemu ya safari yangu katika maisha, nilizoea kuchumbiana na wanaume tofauti ili kupata utegemezo wa kifedha, mmoja alikuwa akinilipia kodi, mwingine alikuwa akininunulia vitu na mwingine akanitunza kwa kulipendezesha kabati langu kwa nguo. Lakini kwa sasa nimekuwa na watoto wa kutosha. Hakuna maangaiko tena kwangu, nanimeokoka” ameeleza Diana.

Related Articles

Back to top button