Burudani

Nandy: Wasanii bongo mmetisha

ZANZIBAR: MSANII wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga maarufu kama Nandy, amepongeza mshikamano na umoja uliooneshwa na wasanii wa Tanzania katika usiku wa Trace Awards uliofanyika Zanzibar.

Nandy amesema kuwa mshikamano huo ni kiashiria cha mafanikio yanayopatikana kupitia muziki wa Bongo Fleva, huku akisisitiza kuwa tasnia hiyo imepiga hatua kubwa.

“Jinsi wasanii wa Tanzania tulivyojitokeza Zanzibar, nadhani mnaona hatujajitokeza kinyonge. Tumeonesha kuwa muziki wetu unalipa, na mafanikio yanaonekana. Mfano mzuri ni Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, alivyoingia na magari yake, akionesha hadhi ya muziki wa Tanzania,” amesema Nandy.

Aidha, amesisitiza kuwa tuzo hizo zimeitangaza Zanzibar kimataifa na kutoa fursa kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana na wenzao wa mataifa mengine katika biashara ya muziki.

Ameongeza kuwa amefanya mazungumzo na msanii Rema hivyo mashabiki zake watarajie lolote kutoka kwao hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button