Ligi Kuu

Azam FC yamweka Feisal Salum kwenye kiti cha Ufalme

DAR ES SALAAM: KLABU ya Azam FC imempa ufalme kiungo mshambuliaji wake Feisal Salum, baada ya kufikisha mabao 10 na kutoa pasi nane za mabao (assists) msimu huu Ligi ikiwa bado inaendelea.

Feisal ameng’ara katika michezo ya Ligi iliyofuatana hivi karibuni akihusika kufunga na kutoa pasi za mabao. Katika mchezo wa jana dhidi ya Namungo aliifungia timu yake bao 1-0.

Feisal, ambaye amekuwa tegemeo kubwa ndani ya kikosi hicho, ameonesha kiwango cha juu kilichomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi wa ligi kwa sasa.

Ubunifu wake uwanjani, uwezo wa kupiga pasi za mwisho pamoja na kufumania nyavu mara kwa mara, vimemuweka katika nafasi ya “kifalme” ndani ya Azam.

Kwa takwimu hizo, nyota huyo ameendelea kuwa mhimili muhimu wa mafanikio ya timu hiyo, huku mchango wake ukionekana wazi katika ushindi na matokeo chanya ya Azam katika michezo mbalimbali ya ligi.

Amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake ambayo katika michezo 21 iliyocheza imefikisha pointi 43 ikiwa katika nafasi ya pili.

Ingawa nafasi ya pili wanaweza wasidumu kutokana na kulingana pointi sawa na wekundu wa Msimbazi Simba waliopo nyuma mchezo mmoja ambao kama watashinda dhidi ya JKT Tanzania leo wataishusha Azam FC hadi nafasi ya tatu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button