Ligi Kuu

Fadlu awawashia moto akina Mukwala

DAR ES SALAAM: Licha ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya KMC FC,  Kocha wa Simba, Fadlu Davids amesema hajafurahishwa na washambuliaji wake kushindwa kutumia nafasi hasa kipindi cha kwanza.

Amesema  kwenye michezo mingi kipindi cha kwanza huwa wanatengeneza nafasi nyingi  kama ilivyo kwa mchezo wa jana lakini washambuliaji wake wanashindwa kuzibadili nafasi hizo kuwa mabao.

“Bado tunatakiwa kufanyia kazi safu ya ushambuliaji,  tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza na kushindwa kufunga, mfano leo (jana) kipindi cha pili KMC FC walikuwa vizuri licha ya kufungwa walicheza vizuri, “ amesema.

Fadlu amesema kila mchezaji anaelewa jukumu zaidi ya nafasi yake anayocheza kiwanjani na kila mmoja anapata nafasi ya kucheza na kumpa anachokitaka.

“Hii ni asilimia 25 ya Simba ninayoitaka nahitaji kuijenga timu imara na kila mchezaji anakuwa muhimu kwenye timu lakini pia kucheza kitimu na hakuna bora ndani ya kikosi changu kila mmoja ana mchango wake muhimu,” amesema kocha huyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button