
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili Dar es Salaam na Dodoma.
Azam itakuwa uwanja wa nyumbani wa Azam Complex kuikaribisha Mtibwa Sugar ambayo itataka kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho timu hizo kukutana Aprili 7, 2023.
Katika mchezo mwingine Singida Fountain Gate itakuwa ugenini dhidi ya Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.