Masumbwi

Kiduku: Mafanikio ya Ibrahim Class yatupa Moyo

DAR ES SALAAM: BONDIA Twaha Kassim ‘Kiduku amesema wao kama mabondia wametoka Morogoro hadi Dar es Salaam kwa lengo la kumpongeza Ibrahim Class kufuatia mafanikio yake makubwa aliyoyapata nchini Thailand kwa kutwaa mikanda miwili ya WBC.

Kiduku na Karim Mandonga ni miongoni mwa mabondia waliojitokeza Jana kumpokea Class aliyepata mapokezi ya kifalme baada ya kufanya vizuri mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kiduku amesema ushindi huo si heshima kwa Class pekee, bali ni fahari kwa Tanzania nzima, huku ukitoa hamasa kwa mabondia wengine kuongeza bidii katika mazoezi ili kufikia mafanikio kama hayo.

Ameongeza kuwa mafanikio ya Class yanawapa moyo mkubwa na kuwafungua njia ya kuamini kuwa inawezekana kutwaa ubingwa ndani na nje ya nchi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili waendelee kufanya vizuri na kulinda heshima ya taifa kwenye ndondi.

Kiduku ana muda mrefu hajacheza pambano la kimataifa nje ya nchi. Mara ya mwisho tangu alipopigwa na bondia wa Ujerumani Juergen Doberstein mwaka juzi alishuka kiwango kidogo.

Related Articles

Back to top button