Masumbwi

Mafia : Hii ilikuwa pasha pasha tu

DAR ES SALAAM:BAADA ya kumchapa mpinzani wake, Prasitsak Phaprom kutoka Thailand, Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Mafia amesema mchezo huo ni kipimo cha kujiandaa na pambano lililo mbele yake ya kuwania mkanda wa WBC.

Mafia usiku wa kuamkia leo ameshinda kwa KO raundi pili baada ya kumchakaza mpinzani wake, Prasitsak pambano raundi 10 uzito wa kati (kilo 53) uliofanyika ukumbi wa City Centre, Magomeni Sokoni, Dar es Salaam.

Ibrahim Mafia amesema juhudi alizofanya na kusikiliza maelekezo ya kocha wake, Hamisi Mwakinyo amefanikiwa kupata ushindi huo wa raundi ya pili

“Prasitsak ni kipimo kwangu kwa ajilu ya kujiandaa na pambano lijalo litakalocheza Oktoba mwaka huu na bondia kutoka Qatar wa kuwania mkanda wa WBC,” amesema Ibrahim Mafia.

Naye kocha wa bondia huyo, Hamis Mwakinyo amesema haikuwa kazi rahisi kumpiga Prasitsak raundi ya pili ni baada ya kumfatilia mpinzanu huyo na kijana wake kufuata kile alichomuelekeza mazoezini.

“Mapambano yameenda vizuri nashukuru kuona bondia wangu amepambana na kuonyesha kile ambacho mashabiki na watanzania wanahitaji,” ameeleza kocha huyo.

Pambano za utangulizi ambapo Salim Kassim aliyeshinda kwa point kwa kumchapa Albert Kimario kutoka Kenya, Richard Mtangi alishinda kwa TKO dhidi ya Christopher Magambo kuumia bega la kulia Ramadhani Kimoko alishinda kwa pointi dhidi ya Harvey Mkacha kutoka Malawi wakati Yohana Mchanja alimpiga kwa pointi Joseph Akai kutoka Ghana.

Related Articles

Back to top button