Kwingineko

‘Uzuri pekee hauwezi kumsaidia mwanamke’

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO Jasinta Makwabe ametoa rai kwa mabinti kutojitegemea kwenye uzuri wao pekee, akisisitiza umuhimu wa kuwa na akili na uwezo binafsi.

Amesema kuwa uzuri bila maarifa na juhudi hauwezi kumsaidia mtu kujitegemea maishani.

Jasinta amesema kuwa binti anayejikita kwenye uzuri tu bila kuwekeza kwenye maendeleo ya kiakili na kiuchumi anajiweka katika hatari ya kushindwa kujimudu kimaisha.

“Ninaamini uzuri pekee hauwezi kulipa bills. Ni muhimu kwa binti kuwa ‘smart’ kichwani na kujituma ili kufikia mafanikio,” amesema Jasinta Makwabe.

Amesisitiza kuwa elimu, ubunifu, na bidii ni mambo muhimu yanayoweza kumuinua mtu, badala ya kutegemea muonekano wa nje pekee.

Related Articles

Back to top button