Kwingineko

Ranieri akilala ukocha, akiamka ukocha.

MILAN: Kocha wa zamani wa Leicester City aliyetangaza kustaafu huenda akarejea uwanjani baada ya kutangaza kurejea ikiwa atapata kazi kwenye timu za taifa.

Ranieri alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya England mwaka 2016 pamoja na kuzifundisha klabu za Chelsea, Juventus, Atletico Madrid, Inter Milan Monaco kabla ya kutangaza kustaafu mwezi Mei.

“Ni kweli natamani kurejea tena kwenye ‘Touch line’ ingawa nimekataa zaidi ya ofa moja, Wacha tuone kama simu itatoka kwenye timu ya taifa ” kikongwe huyo mwenye miaka 73 aliliambia gazeti la kila siku la Corriere della Sera, Italy.

Ranieri Alikataa pia kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Italy, akisema kwa wakati ule alikuwa na imani kubwa na meneja wa sasa wa wa timu ya taifa ya Italy ‘Azzurri’ Luciano Spalletti.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button