Nyumbani

Singida kuivaa Mlendege kwa tahadhari

ZANZIBAR: KOCHA Mkuu wa Singida Black Stars, Muhibu Kanu, amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Muungano dhidi ya Mlandege kesho, akisisitiza kuwa maandalizi yamekamilika kwa lengo la kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kanu amesema licha ya kuutambua ugumu wa mechi hiyo, wamejipanga ipasavyo kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

“Tumefanya maandalizi mazuri na kikosi chetu kipo kamili. Tunajua itakuwa mechi ngumu kwa sababu Mlandege ni moja ya timu kongwe yenye mashabiki wengi, hivyo tunatarajia ushindani mkubwa uwanjani,” amesema Kanu.

Ameongeza kuwa wamewaandaa wachezaji wao kisaikolojia kukabiliana na presha ya mashabiki pamoja na mazingira ya mchezo huo.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu, tunafahamu ubora wao uko wapi na mapungufu yao yako wapi. Kilichobaki ni kuwaelekeza wachezaji wetu namna bora ya kutumia nafasi hizo ili kufikia malengo ya klabu,” ameongeza.

Singida Black Stars inatarajia kutumia mchezo huo kama sehemu ya kuthibitisha ubora wao na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye mashindano ya Kombe la Muungano.

Related Articles

Back to top button