LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili ya ‘Derby’ za timu za jeshi na wazalishaji wa sukari zitakazofanyika Dar es Salaam na Kagera.
Maafande wa JKT Tanzania inayoshika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 19 itawaalika maafande wenzao wa Tanzania Prisons iliyopo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 27 baada ya michezo 20 kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni.
Kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, walima miwa wa Turiani, Morogoro, Mtibwa Sugar iliyopo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 19 itakuwa mgeni wa walima miwa wenzao Kagera Sugar inayoshika nafasi ya 9 ikiwa na pointi 23 baada ya michezo 20.