Ligi KuuNyumbani

Patashika Prisons vs Coastal leo

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Mbeya na Lindi.

Maafande wa Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Coastal Union kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku kila timu ikihitaji ushindi kujiweka sawa.

Coastal na Prisons zote zina pointi saba kila moja zikishika nafasi ya 14 na 15 baada ya michezo tisa.

Ihefu itakuwa mgeni wa Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa mjini Lindi huku zote zikiwa na pointi nane kila moja.

Namungo ipo nafasi ya 11 wakati Ihefu inashika nafasi 13 baada ya michezo tisa kila moja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button