Maandalizi ya tamasha la sarakasi Tanzania yaanza rasmi

DAR ES SALAAM: WATAALAM kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) leo wamekutana na viongozi wa Chama cha Sarakasi Tanzania (CHASATA) kujadili maandalizi ya kuanzishwa kwa Tamasha la Sarakasi nchini.
Akizungumza na SpotiLEO Mkurugenzi Msaidizi wa Tafiti na Masoko wa BASATA Mrisho Mrisho katika ukumbi wa mikutano wa BASATA uliopo Dar es Salaam, wataalamu wa sanaa pamoja na wawakilishi wa chama hicho cha sarakasi.
Lengo la mkutano huo lilikuwa kujadili hatua za awali za kuanzisha tamasha la sarakasi litakalolenga kukuza na kuendeleza sanaa ya sarakasi nchini, pamoja na kuwapa wasanii jukwaa la kuonesha vipaji vyao.
“Washiriki wa kikao walibadilishana mawazo kuhusu namna bora ya kuandaa tamasha hilo, ikiwa ni pamoja na ratiba, ushirikiano wa wadau mbalimbali wa sanaa, na mikakati ya kuhakikisha tamasha hilo linakuwa endelevu.”amesema Mrisho
Inatarajiwa kuwa tamasha hilo litasaidia kuhamasisha maendeleo ya sanaa ya sarakasi nchini na kuongeza fursa kwa wasanii wa sarakasi kujitangaza ndani na nje ya Tanzania.




